21 messages over 3 pages: 1 2 3 Next >>
strikingstar Bilingual Tetraglot Senior Member United States Joined 5177 days ago 292 posts - 444 votes Speaks: English*, Mandarin*, Cantonese, Swahili Studies: Spanish, Arabic (Written)
| Message 1 of 21 29 September 2010 at 3:28am | IP Logged |
Karibuni. Njoo hapa na uache ujumbe kama unaweza kusema Kiswahili.
Hapa, tunaweza kujadili chochote ulimwenguni. Lakini kwanza, tujijulishe na tuzungumze
kuhusu kwa nini tunapenda Kiswahili na kwa nini tunataka kujifunza lugha hii. Pia,
tujaribu kutumia Kiswahili tu kwa hiyo sisi sote tunaweza kuboresha pamoja.
Nitaanza. Nilijifunza Kiswahili miaka miwili iliyopita nilipoenda Tanzania. Nilianguka
katika upendo na Tanzania, watu yake na lugha yake. Baada ya niliondoka Tanzania,
nikaendelea kujifunza Kiswahili katika chuo kikuu. Sasa, nimehitimu na nimekuwa
kujifundisha Kiswahili kwa sababu ninatamani kurudi Tanzania siku moja. Ninatumaini
kusikia toka kila mtu mwingine.
Asante.
1 person has voted this message useful
| ellasevia Super Polyglot Winner TAC 2011 Senior Member Germany Joined 6146 days ago 2150 posts - 3229 votes Speaks: English*, German, Croatian, Greek, French, Spanish, Russian, Swedish, Portuguese, Turkish, Italian Studies: Catalan, Persian, Mandarin, Japanese, Romanian, Ukrainian
| Message 2 of 21 01 October 2010 at 4:28am | IP Logged |
Hujambo strikingstar!
Bado siwezi kusema Kiswahili vizuri sana, lakini ninapanda sana lugha hii na nimefurahi sana kuweza kukufahamu (sikujui maneno machache tu). Nilianza kujifunza Kiswahili takriban miezi saba iliyopita kwa sababu niliziua kwamba ukoo wangu watakwenda Tanzania Julai. Zamani nilitaka kujifunza lugha hii kwa sababu nilifikiri kwamba ni ya kuvutia na nzuri sana, lakini sikuwa na sababu nyingine njema. Sikusoma sana miezi mikwanza mitatu, lakini ulipoisha mwaka ya shule nilikuwa na mara zaidi nisome.
Tulipoenda Tanzania takriban miezi mitatu iliyopita, tulijistarehesha sana. Tulitembelea maeneo makuu mengi kama vile Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Ngorongoro, Serengeti, na kadhalika. Pia, tulitembelea kijiji cha Wamaasai na shule ya msingi, na nilisema nao kwa Kiswahili. Watu wote walikuwa wa kirafiki sana, na ulikuwa uzoefu wa ajabu kuweza kuzungumza nao kwa lugha yao—na wao, hawakuweza kuamini kwamba Mzungu kijana walitaka kuijifunza! Bila shaka walinisaidia sana.
Baada ya safari nilitaka kuendelea kuisoma kwa sababu nilizipenda sana nchi na lugha, lakini silikuwa na mara na silisoma sana tangu mwanzo wa Agosti, nilipokiisha kitabu changu cha kipenzi (kinachoitwa "Spoken World Swahili"). Kwa hivyo nimesahau maneno mengi na kanuni ya sarufi nyingi. Hata hivyo ninaanza kuijifunza tena, na ninatumai kukumbuka kila kitu.
Ninatumai utaweza kunifahamu, na ninayashukuru marekebisho. Asante na tutaonana!
P.S. Karibu tovuti!
Edited by ellasevia on 01 October 2010 at 4:31am
1 person has voted this message useful
| strikingstar Bilingual Tetraglot Senior Member United States Joined 5177 days ago 292 posts - 444 votes Speaks: English*, Mandarin*, Cantonese, Swahili Studies: Spanish, Arabic (Written)
| Message 3 of 21 01 October 2010 at 7:04am | IP Logged |
Hujambo ellasevia. Ukoje? Mimi sijambo.
Asante sana kwa kuitikia ujumbe wangu. Nimeanza kufikiri kwamba hakuna mtu asemaye
Kiswahili hapa. Unajua Kiswahili vizuri sana na nilielewa vitu ambavyo uliandika.
Usihangaike. Labda tunaweza kusaidiana kuboresha. Itakuwa nzuri kama unaweza
kusahihisha makosa yangu na ninaweza kusahihisha makosa yako. Unafikirije?
Inaonekana kwamba ulikuwa na mara nzuri katika Tanzania. Ninafurahi kwa wewe. Mimi
ninapenda Tanzania sana vile vile. Kwa nini ulienda Tanzania? Kusafiri tu? Au
ulifanya kazi katika Tanzania pia? Nilienda Tanzania kujitolea katika hospitali St.
Elizabeth mjini Arusha. Mimi ni mhandisi na nilienda na shirika inaloitwa EWH.
Nilitengeneza mashine ambazo ziliharibika katika hospitali. Ni kazi ya kuvutia na
nilifurahia sana.
Nilitembelea maeneo makuu chache pia, kama Ngorongoro, kisiwa cha Zanzibar na mlima
wa Kilimanjaro. Nilitaka kuenda maeneo mengine kama Serengeti na mziwa wa Victoria
lakini yao ni mbali sana na sikuwa na nafasi. Angalau, nina sababu kurudi Tanzania siku
moja. Je, ulienda Zanzibar au ulipanda Kilimanjaro?
Edited by strikingstar on 01 October 2010 at 8:52pm
1 person has voted this message useful
| ellasevia Super Polyglot Winner TAC 2011 Senior Member Germany Joined 6146 days ago 2150 posts - 3229 votes Speaks: English*, German, Croatian, Greek, French, Spanish, Russian, Swedish, Portuguese, Turkish, Italian Studies: Catalan, Persian, Mandarin, Japanese, Romanian, Ukrainian
| Message 4 of 21 02 October 2010 at 6:09am | IP Logged |
Strikingstar,
Mimi pia sijambo, lakini katika Tanzania sikusikia hakuna mtu anenaye “hujambo” au “sijambo.” Wote walinena “jambo” au “mambo” na lazima ujibu “poa.” Walinisema kwamba ni misimu.
Asante, nilifikiri kwamba Kiswahili yangu ni mbaya sana! Sijui kama nitaweza kukusahihishia makosa yako lakini nitajaribu nikiyaona! Ninajua kwamba kuna watu ambao wanasoma Kiswahili hapa, lakini kwa bahati mbaya hakuna wengi kwa sababu lugha za Afrika si maarufu sana hapa. Labda watakuja hapa wazungumze nasi.
Ndio, safari ilikuwa ya ajabu. Tulienda hapo kwa ajili ya kuadhimisha siku ya ndoa ya ishirini ya wazee wangu. Walienda Afrika miaka ishirini iliyopita, na walitaka kurudi pamoja na wana wao (mimi na ndugu yangu) kwa sababu wanapenda sana Afrika, hasa Afrika ya Mashariki. Hatukufanya kazi katika Tanzania, lakini marafiki yetu, walioenda Kenya takriban miaka sita iliyopita, walifanya kazi shuleni lakini hawakuweza kuona nchi na wanyama. Ninataka kurudi Afrika ya Mashariki (na maeneo ya Afrika mengine), na labda nitajitolea shuleni—ingekuwa njema sana kwa Kiswahili yangu.
Tulitembelea mji Arusha—unaonekana mji mzuri lakini hatukufanya vitu vyingi hapo. Nilitaka sana kutembelea kisiwa cha Zanzibar lakini baba yangu hakuweza (ninafikiri pia kwamba hakutaka kwenda). Ninafikiri kwamba yeye alikuwa na mambo ya kazi (mkutano?) hapa na kwa bahati mbaya hatukuwa na muda. Walipoenda Afrika miaka ishirini iliyopita, wazee wangu walipanda mlima wa Kilimanjaro lakini mara hii hatukuupanda.
Ninakushukuru sana kwa kufungua mazungumzo haya. Sasa ninataka kusoma na kusema Kiswahili tena! Asante sana!
Edited by ellasevia on 03 October 2010 at 8:27am
1 person has voted this message useful
| strikingstar Bilingual Tetraglot Senior Member United States Joined 5177 days ago 292 posts - 444 votes Speaks: English*, Mandarin*, Cantonese, Swahili Studies: Spanish, Arabic (Written)
| Message 5 of 21 05 October 2010 at 10:49pm | IP Logged |
Hujambo Ellasevia,
Labda watu uliwaokutana katika Tanzania hawakuutarajia kuweza kusema Kiswahili, kwa
hiyo walitumia "Mambo" au "Jambo" kuuamkia. Tokea hapo, maneno haya ni "Sheng" (aka
Swahili slang.) Hapo awali, nilipoenda Tanzania, watu wote waliniamkia na "Sheng" pia.
Lakini, baada ya nilijifunza zaida ya Kiswahili, nikakataa kuzungumza na "Sheng" kwa
sababu sikusikia hii ni Kiswahili halisi. Ninasikia kama tunawaonyesha kwamba tunasema
Kiswahili, tunaweza kuwa na zaida ya mazungumzo yenye maana.
Ni nzuri sana ulisafiri Afrika Mashariki na jamaa yako. Pia, ninafurahi tulienda
Arusha. Arusha ndio mji mzuri na nina rafiki nyingi pale. Ingawa watu wengi hutumia
Arusha kuenda mahali ya muhimu mengine, Arusha bado ina mahali ya ajabu ya chache, kama
mlima wa Meru, hifadhi ya Arusha na migodi ya Tanzanite na kadhalika. Nilifurahia
kuishi katika Arusha. Watu wa Arusha ni wazuri na wapole na maisha yalikuweko salama.
Nitahitaji kurudi kabisa.
Ulijifunza Kiswahili jinsi gani? Unasoma shuleni? Au unajifundisha? Hakuna rasilimali
nyingi kwa Kiswahili katika interneti. Japo, nilipenda kutumia tovuti ambayo inaitwa
"Mwana Simba" nilipoanza kujifunza Kiswahili. Pia, nilitumia kitabu ambacho kinaitwa
"Tujifunze Kiswahili" nilipochukua somo la Kiswahili shuleni. Kitabu kinaandikwa na
mwandishi anayeitwa Mugane.
Ninafurahi sana kuzungumze nawe pia. Kwa kweli, nilijiunga tovuti hii ni kwa sababu
nilitafutia wasemaji wa Kiswahili. Juzi juzi, nilikuwa kulenga Kiarabu na Kihispana.
(Kiarabu ni kigumu sana sana sana ijapo Kiswahili kinakopa maneno mengi toka Kiarabu.)
Lakini, sitaki nisahau Kiswahili. Mazungumzo yake yaliboresha Kiswahili changu na
ninakushukuru pia.
Asante na tutaonana baadaye.
1 person has voted this message useful
| ellasevia Super Polyglot Winner TAC 2011 Senior Member Germany Joined 6146 days ago 2150 posts - 3229 votes Speaks: English*, German, Croatian, Greek, French, Spanish, Russian, Swedish, Portuguese, Turkish, Italian Studies: Catalan, Persian, Mandarin, Japanese, Romanian, Ukrainian
| Message 6 of 21 07 November 2010 at 9:44am | IP Logged |
Hujambo strikingstar,
Samahani sikujibu ujumbe wako--uliuandika mezi moja iliyopita! Nimeshughulika sana sana na sikuwa na nafasi kukujibu. Kwa bahati mbaya nimesahau maneno mengi na kanuni za sarufi chache kwa Kiswahili, kwa hivyo sasa Kiswahili changu bila shaka si kizuri sana. :(
Ninasoma Kiswahili tu -- bado siwezi kukisema. Sisomi lugha hii shuleni kwa sababu bado ninasoma shuleni ya sekondari (nina miaka kumi na sita), na shule yangu hana msomo wa Kiswahili. Ina misomo ya Kihispana, Kifaransa, Kirumi, Kijerumani, na Kijapani tu, na ninachukua masomo ya Kijerumani na Kijapani. Kwa hivyo ninajifundisha Kiswahili pekee. Ninatumia vitabu viwili: "Spoken World: Swahili" na "Teach Yourself Swahili," lakini nimekwisha tayari kitabu cha kwanza. Kwamba nisome msiamati hutumia programu ya kompyuta inayoitwa "Anki." Ni njema sana, unaijuaje? Pia, hutumia tovuti kwamba uliitwa, "Mwana Simba." Ninafikiri kwamba nitatumia pia kitabu ya Assimil, "Le Swahili Sans Peine," kinachoandikwa kwa Kifaransa. Ninapenda vitabu vya Assimil, na ninatumai kwamba pia kitabu hiki kitakuwa chema.
Kihispana ni Kizungu chako cha kwanza (zaidi ya Kiingereza), kweli? Unafikirije? Tayari ulijifunza Kikantoni na Kiswahili, vinavyokuwa lugha za Asia na Afrika. Kihispana ni kigumu au rahisi kwa wewe? Vizungu ni tofauti sana na lugha za Afrika na Asia, na hivyo nilitaka kukuuliza.
Ninataka kujifunza Kiarabu pia na ninafurahi sana kwamba kuna maneno mengi kutoka Kiarabu yaliyokopwa na Kiswahili kwa sababu ninajua maneno ya Kiarabu machache sasa! Ninajifunza Kiajemi pia na ninaweza kubaini maneno mengi kutoka Kiswahili (lakini ni kutoka Kiarabu). Kwa mfano wiki chache iliyopita nilijifunza neno la Kiajemi "دقیقه" (daqiqe) lenye maana ya "minute." Nikafikiri kwamba neno hili lilionekana zoevu...na nikakumbuka meno la Kiswahili kwa "minute" -- dakika! Lugha ni za kisisimua sana. :) Ninatumai kwamba nitapoanza kusoma Kituruki itakuwa sawa na hivyo, kwa vile ni lugha ya Mashariki ya Kati pia.
Haya basi ninafikiri kwamba nimeandika ya kutosha kwa leo usiku. Kama utaweza kuona makosa yangu, tafadhali uyasahihishe tafadhali!
Usiku mwema,
ellasevia
Edited by ellasevia on 07 November 2010 at 9:46pm
1 person has voted this message useful
| strikingstar Bilingual Tetraglot Senior Member United States Joined 5177 days ago 292 posts - 444 votes Speaks: English*, Mandarin*, Cantonese, Swahili Studies: Spanish, Arabic (Written)
| Message 7 of 21 29 November 2010 at 6:51am | IP Logged |
Habari zako, ellasevia.
Pole sana. Sikutambua kwamba uliniitikia. Wow, wewe ni kijana sana. Niliwaza wewe
ulikuwa mkubwa kuliko kumi na sita. Ni nzuri sana kwamba una shauku kwa lugha ingawa
wewe bado ni shababi. Ninasikia kama mzee wakati ninakulinganisha. Nilitamani nikaanza
kujifunza lugha nyingine mapema zaidi maishani mwangu.
Kiingereza ni lugha yangu ya kwanza. Kikantoni ni lugha yangu ya pili na nilijifunza
Kichina kwa miaka kumi shuleni wakati nilikuwa nikikua. Kwa hivyo, niliweza kulinga
Kiswahili, Kihispana na Kiarabu tu. Ninadhani Kihispana na Kiswahili ni sawa. Lakini,
Kiarabu ni kigumu sana sana sana (see previous post) kwa sababu Kiarabu kina kanuni za
sarufi nyingi ambazo ni illogical sana. Msamiati ni kigumu pia, kwa ajili umoja na
wingi kwa maneno mengi ni tofauti sana. Lazima niboreshe Kiarabu changu kabisa.
Ninahitaji kutia juhudi kukijifunza. Bado nina barabara refu kuenda.
Unajua lugha nyingi, unasikia lugha iliyo kigumu ni gani? Na lugha ambayo unapenda
iliyo mwema sana ni gani?
Edited by strikingstar on 29 November 2010 at 7:40am
1 person has voted this message useful
| ellasevia Super Polyglot Winner TAC 2011 Senior Member Germany Joined 6146 days ago 2150 posts - 3229 votes Speaks: English*, German, Croatian, Greek, French, Spanish, Russian, Swedish, Portuguese, Turkish, Italian Studies: Catalan, Persian, Mandarin, Japanese, Romanian, Ukrainian
| Message 8 of 21 29 November 2010 at 7:59am | IP Logged |
Nimeshapoa, strikingstar. Habari zangu sizo mbaya, lakini nimeshughulika sana. Habari zako?
Ndio, mimi si mzee! Asante sana. Nilianza kusoma lugha za kigeni peke yangu nilipokuwa na miaka kumi na mimoja. Nilianza kusoma Kihispana shuleni ya msingi ya kusema lugha mbili nilipokuwa na miaka mitano tu. Kigiriki ni lugha ya ukoo wangu, na nilikisikia nyumbani nilipokuwa mtoto mdogo. Nilianza kukisoma nilipokuwa na miaka saba (na halafu, miaka na miwili). Hakikuwa kigumu kwa mimi kwa vile kilikuwa kama lugha ya kwanza ya sekondari. Halafu, nilipokuwa na miaka kumi na mimoja nikajaribu kusoma Kichina, lakini kilikuwa kigumu sana kwa sababu ya matamshi na sauti. Mwaka ya pili nikaanza kusoma Kifaransa na Kireno na vilikuwa rahisi sana kwa sababu nilijua tayari Kihispana vifasaha. Kitaliana kikakuwa sawa. Kijerumani kilikuwa lugha yangu ya kwanza niliyoanza kwa shida. Kiswahili kilikuwa lugha yangu ya kumi na moja, nadhania.
Sifahamu vizuri sana historia yako ya lugha. Kiingereza ni lugha yako ya kwanza lakini ukajifunza Kikantoni pia (kilisemwaje nyumbani?) na ulijifunza Kichina shuleni? Ninaona kwamba unasoma Kijapani pia. Unafikirije?
Ninafikiri lugha gani ni kigumu? Kijapani ni kigumu, lakini nakipenda sana sana sana na ukisema lugha haidhuru kama ni gumu. Kirusi (na Kiswahili pia kidogo) ni kigumu, lakini tena, nakipenda sana. Awali Kijerumani kilikuwa kigumu lakini sasa ni rahisi zaidi kabisa!
Napenda lugha nyingi, lakini baadhi ya vipenzi vyangu ni Kigiriki, Kijapani, Kirusi, Kiarabu, Kiswahili, Kicheki, na Kifini.
Tutaonana!
Philip (ellasevia)
Edited by ellasevia on 29 November 2010 at 10:08am
1 person has voted this message useful
|
This discussion contains 21 messages over 3 pages: 1 2 3 Next >>
You cannot post new topics in this forum - You cannot reply to topics in this forum - You cannot delete your posts in this forum You cannot edit your posts in this forum - You cannot create polls in this forum - You cannot vote in polls in this forum
This page was generated in 0.6250 seconds.
DHTML Menu By Milonic JavaScript
|